Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kijana mjasiriamali ajikimu katikati ya changamoto za COVID-19 ukimbizini Uganda 

Kijana mjasiriamali ajikimu katikati ya changamoto za COVID-19 ukimbizini Uganda 

Pakua

Vijana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC) walioko ukimbizini nchini Uganda hutumia muziki kuleta matumaini na wakati huo huo kuchagiza amaani na upendo miongoni mwa wakimbizi katikati ya changamoto lukuki ukimbizini kuanzia malazi, chakula na mahitaji mengine. 

Kando na hilo vijana wenye busara wametumia kipaji hicho cha kitamaduni miongoni mwao kujipatia umarufu na pia kuwasaidia kupata fursa za kibiashara. Mfano ni kijana, Idi Nasibu Davis katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali anayetunga nyimbo zake huku vile vile akitumia kipaji chake cha kutengeneza watu kucha na kuwapaka rangi ili kujipatia kipato na kuondokana na umaskini. Kwa kina basi ya kile afanyacho na ujumbe wake kwa wakimbizi wenzake, ungana na mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego aliyekutana naye ndani ya makazi hayo ya wakimbizi. Kijana huyu amejulikana sana pia na kazi yake kama “Cutex-man”. 

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Sauti
3'53"
Photo Credit
John Kibego