Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 Desemba 2021

09 Desemba 2021

Pakua

Karibu kusikiliza jarida, mwenyeji wako ni Flora Nducha anayekujuza kwa undani kuhusu. 

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imesema janga la coronavirus">COVID-19 limeleta hali mbaya zaidi kwa watoto kuwahi kushuhudiwa katika historia yake ya miaka 75 nakuzitaka nchi kuongeza juhudi kuwanusuru watoto.

Machafuko yanayoendelea katika jimbo la Darfur nchini Sudan yamewasababisha maelfu ya watu kufungasha virago na kuyakimbia makazi yao tangu mwezi Novemba mwaka huu, wengi wakitawanywa ndani ya nchi na wengine kwenye mpaka wa nchi Jirani ya Chad limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na kuongeza kuwa linatiwa hofu kubwa na hali hiyo.

Siku kama ya leo tarehe 9 mwezi Desemba mwaka 1961, iliyokuwa Tanganyika au Tanzania Bara ilipata Uhuru wake kupitia mchakato uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa. Siku 5 baadaye, nchi hiyo huru ilijiunga na Umoja wa Mataifa na kuwa mwanachama hadi leo na hii leo inaposherehekea miaka 60 ya uhuru wake, pia inatambua faida inazozipata kwa kuwa mwanachama wa UN kama anavyoeleza Kaimu Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Songelael Shilla alipozungumza na Idhaa hii jijini New York Marekani.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'15"