Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni za nyumba kwa nyumba, eneo kwa eneo zatokomeza Polio Afrika

Kampeni za nyumba kwa nyumba, eneo kwa eneo zatokomeza Polio Afrika

Pakua

Polio! Polio! Polio! Ugonjwa uliokuwa ukilemaza watoto 75,000 kila mwaka wakati wa miaka ya 1990 katika nchi za Afrika wanachama wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika. Mataifa hayo ni 47 barani Afrika isipokuwa Somalia, Sudan, Eritrea, Misri, Libya na Tunisia. Gonjwa hilo halina tiba bali lina kinga ambayo ni chanjo, kinga ambayo viongozi kuanzia wa kaya hadi kimataifa walisimamia kidete kuhakikisha inamfikia kila mtoto barani Afrika na tarehe 25 mwezi huu wa Agosti, ukanda huo umetangazwa kuwa hakuna tena Polio! Nini kimefanyika? Ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Audio Credit
Loise Wairimu/ Assumpta Massoi
Audio Duration
3'58"
Photo Credit
© UNICEF/Karin Schermbrucke