Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wakosa mgao wa chakula kufuatia marufuku ya usafiri wa umma, Uganda

Wakimbizi wakosa mgao wa chakula kufuatia marufuku ya usafiri wa umma, Uganda

Pakua

Nchini Uganda kama ilivyo katika maeneo mengine duniani imeimarisha hatua za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Corona au COVID-19 kutokana na  ongezeko la wagonjwa.

Hatua hizo zikiwa ni pamoja na kufunga tasisi zote za elimu na kupiga marufuku usafiri wa umaa vimekuwa na madhara makubwa hususan kwa wakimbizi katika nchi hiyo yenye wakimbizi zaidi ya milioni 1.3.  

Idadi ya wagonjwa wa COVID-19  imeongezeka na kufia 33 kwa mujibu wa shirika la afya la nchi hiyo. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amemtembelea mmoja wa wakimbizi mjini Hoima Access Bazibuha Mudosia kutoka Jmahuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), aliyejikuta amekwama na kushindwa kurejea kambini Kyangwali baada ya kufungwa usafiri wa umma  

(Mahojiano kati ya Kibego na Bazibuha)

Audio Credit
Loise Wairimu/ John Kibego
Audio Duration
3'45"
Photo Credit
WFP