Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtandao wa Twitter umeiwezesha IBUA Afrika kuwasaidia vijana: Mumbi

Mtandao wa Twitter umeiwezesha IBUA Afrika kuwasaidia vijana: Mumbi

Pakua

Katika zama hizi ambazo kunashuhudiwa mabadiliko katika teknolojia na hata matumizi ya mitandao ya kijamii na huku kuiwa na mwamko wa vijana kujitokeza kuwa wabunifu na kudhihirisha ajira si lazima kuajiriwa  , vijana wameanzisha miradi mbali mbali wakitumia mitandao ya kijamii na teknolojia za kisasa na ambazo zimewasaidia kubadili maisha yao na kuletea kipato. 

Nchini Kenya kijana Mumbi Ndung'u ni mwanzilishi wa shirika la IBUA ambalo kiini chake ni mtando wa kijamii wa twitter sasa limekuwa ni jukwaa linaolunganisha vijana na wawekezaji ikiwemo serikali kwa lengo la kusongesha mbele ajenda ya maendeleo na kumfaya kijana kujitegemea.

Basi ili kupata undani wa makala hii ungana na Grace Kaneiya katika mahojiano haya jijini New York Marekani wakati wa jukwaa la vijana lililofanyika hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Sauti
4'4"
Photo Credit
UNnewskiswahili/Patrick Newman