Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Likizo ya uzazi ni haki ya mama na mtoto: Doris Mollel

Likizo ya uzazi ni haki ya mama na mtoto: Doris Mollel

Pakua

Likizo ya uzazi ni haki kwa kila mama anayefanyakazi kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na ni muhimu katika afya ya mama na mtoto lakini zaidi ukuaji wa mtoto. Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la kazi duniani , ILO lililopisha mkataba wa likizo ya uzazi mwaka 1919, suala hili limekuwa changamoto kwa mamilioni ya wazazi katika nchi nyingi duniani kutokana na sheria za kazi zilizowekwa na waajiri wao.

ILO imefanyia marekebisho mkataba huo ulioridhiwa n anchi 185 hadi sasa mwaka 1952 na mwaka 2000 ambapo likizo hiyo ilijumuisha pia baba. Na kwa mujibu wa mkataba mama mzazi anapaswa kupata likizo isiyopungua wiki 14 baada ya kujifungua, baba naye anastahili kupata angalau wiki mbili, lakini pia ulinzi wa kazi yao, ulinzi wa afya zao, makubaliano maalumu katika kipindi cha kunyonyesha na huduma kwa watoto. Kwa pande wa Tanzania suala hili likoje?

Katika makala hii Flora Nducha ameketi na Doris Mollel mmoja wa wanaharakati wa kupigania haki za mama na mtoto kutoka taasisi ya Doris Mollel

Audio Credit
Patrick Newman/ Flora Nducha / Doris Mollel
Audio Duration
5'36"
Photo Credit
UNICEF/Prashanth Vishwanathan