Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkanganyiko wa kisiasa ni changamoto katika elimu ya afya kwa wasichana

Mkanganyiko wa kisiasa ni changamoto katika elimu ya afya kwa wasichana

Pakua

Umoja wa Mataifa kupitia malengo ya maendeleo endelevu SDGs yakijulikana pia kama ajenda 2030, unaendelea  kupigia  chepuo masuala kadhaa muhimu ikiwemo haki za vijana wa kike ili nao wapatiwe fursa sawa kama ilivyo kwa watoto wa kiume. 

Utekelezaji wa hoja hiyo umefika hadi mashinani ukijumuisha mashirika ya kiraia yanayounga mkono kazi za Umoja wa Mataifa. Katika makala ya leo basi Patrick Newman amezungumza na Sofia Donald ambaye ni mratibu wa shirika la Sauti ya Wanawake Ukerewe, nchini Tanzania ambalo limejikita na huduma ya kuwawezesha vijana wa kike vijijini. Katika mazungumzo yao wameangazia fursa na changamoto wanazokumbana nazo katika huduma zao. Kwa kina basi ungana naye katika makala hii.


 

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
4'20"
Photo Credit
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Weruweru nchini Tanzaniwa wakiwa wamebeba mabango ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kutoka namba 1 hadi 5. (Picha: UNRCO/Mariam Simba)