Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVAW yabadili maisha ya wasichana wa kaunti ya Kwale

COVAW yabadili maisha ya wasichana wa kaunti ya Kwale

Pakua

Utalii wasifika sana kwa kuinua kipato cha nchi ya Kenya iliyoko Afrika Mashariki. Hata hivyo baadhi ya watalii wawe wa ndani au wa nje wanatumia fursa hiyo kutekeleza mambo yanayokiuka haki za binadamu hususan kufanya biashara ya ngono. Kutokana na umaskini baadhi ya wasichana kwenye kaunti ya Kwale huko Mombasa, wametumbukia katika mtego wa biashara ya ngono au hata biashara ya binadamu na kujikuta na madhila makubwa zaidi. Shirika moja la kiraia linalopinga ukatili na ghasia dhidi ya wanawake nchini Kenya, COVAW limechukua hatua. Je ni hatua gani? Assumpta Massoi amezungumza na Terry Kunina, afisa program wa uchechemuzi na mawasiliano wa shirika hilo ambaye yuko New York, Marekani akihudhuria mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW62. Terry anaanza kwa kuelezea shirika lao.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
3'53"
Photo Credit
UN News/Patrick Newman