Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMI yaelezea mashaka kufuatia uamuzi wa Iraq kufunga ofisi za Al Jazeera Baghdad

UNAMI yaelezea mashaka kufuatia uamuzi wa Iraq kufunga ofisi za Al Jazeera Baghdad

Pakua

Mpango wa Umoja wa mataifa nchini Iraq UNAMI, umeelezewa hofu yake dhidi ya uamuzi wa tume ya mawasiliano na vyombo vya habari nchini Iraq kutoa amri ya kufunga ofisi za kituo cha Al Jazeera mjini Baghdad.

UNAMI imesema wakati inaheshimu mtazamo wa tume hiyo , lakini wakati wa machafuko na migogoro , vyombo huru hata kama maoni yake ni kinzani au yanapingwa au kutopendwa, vinakuwa muhimu saana katika kutekeleza mashlahi ya umma na kulinda demokrasia.

Photo Credit
Picha:UM/Rick Bajornas