Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa yaweza kuwa kichocheo cha kudhibiti utoaji gesi chafuzi

Madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa yaweza kuwa kichocheo cha kudhibiti utoaji gesi chafuzi

Pakua

Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa unafanyika Doha, Qatar suala kubwa likiwa ni hatua za kuchukua kupunguza gesi chafuzi zinazochochea ongezeko la joto duniani. Wakati hilo likijdaliwa, shirika la mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP, limetoa taarifa inayozungumzia uwezekano wa kuyeyuka kwa kasi kubwa kwa udongo wenye barafu, Permafrost, ulioko kwenye maeneo ya kaskazini mwa dunia kitendo ambacho kitatoa hewa aina ya Methani yenye madhara zaidi kwa dunia kuliko hewa ya ukaa.

Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa alizungumza na mmoja wa washiriki wa mkutano huo Bwana Richard Muyungi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya Sayansi na Taaluma ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi ambaye pamoja na kuelezea madhara alitaja mvutano uliopo na hatua za kuchukua ili kuepusha au kupunguza madhara ya myeyuko huo.

(PKG. YA MAHOJIANO)