Akili Mnemba inarahisisha mambo lakini inahitaji usimamizi - Profesa Pillay
Kila uchao, mikutano ifanyika kona mbali mbali za dunia kubonga bongo ni kwa vipi akili mnemba inaweza kutumika kwa manufaa ya binadamu na si vinginevyo kwani Umoja wa Mataifa unataka nyenzo hiyo iwe ya manufaa hasa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.