10 NOVEMBA 2023
Ungana na Leah Mushi kusikia haya jaridani hii leo:
Hofu ya uhalifu wa vita ikitanda UN yataka jinamizi linaloghubika Gaza liishe.
UNMISS yawajengea wanajeshi wa Sudan Kusini uwezo kulinda haki za watoto.
Ungana na Leah Mushi kusikia haya jaridani hii leo:
Hofu ya uhalifu wa vita ikitanda UN yataka jinamizi linaloghubika Gaza liishe.
UNMISS yawajengea wanajeshi wa Sudan Kusini uwezo kulinda haki za watoto.
Hii leo Jaridani Evarist Mapesa anakuletea mada kwa akina inayoangazia kazi za majumbani na utasikia kisa cha mtoto wa miaka 11 kutoka nchini Tanzania ambaye akiwa na miaka 10 alikuwa akitumikishwa pamoja na madhila mengine aliyokumbana nayo.
Hali kwa raia walioko Ukanda wa Gaza Mashariki ya Kati inazidi kuwa mbayá kila uchao hasa kutokana na kuendelea kwa operesheni za kijeshi za Israel za agani na ardhini zilizosababisha maelfu ya raia kuendelea kutaabika kwa kukosa mahitaji muhimu ya msingi kama chakula, maji, huduma za afya na maw
Catriona Laing, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia amethibitisha kuwa Umoja wa Mataifa unashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Maendeleo ya Wanawake na Haki za Binadamu nchini humo kuhakikisha kwamba sauti za wanawake zinasikika katika Baraza la Ushauri
Tukio la mkondo joto la El Niño linalosababisha hivi sasa mvua kubwa, joto kali na ukame kwenye maeneo mbalimbali ya dunia, linatarajiwa kuendelea duniani na kuchochea ongezeko la kiwango cha joto baharini na ardhini, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO hii leo.
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika mwelekeo wa El Nino ya kwamba itaendelea hadi Aprili 2024, halikadhalika madhara yake, Somalia kulekea uchaguzi mkuu na ushiriki wa wanawake; Makala inabisha hodi Mashariki ya Kati usaidizi wa kibinadamu huko Gaza, na mashinani inabisha hodi
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa ulikuwa na siku tano za kuadhimisha Umoja wa Mataifa kutimiza miaka 78 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945 huko San Fransisco nchini Marekani. Maadhimisho yalifanyika kuanzia tarehe 23 hadi 27 Oktoba kwenye mji mkuu, Kinshasa.
Vijana wana dhima kubwa katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayofikia ukomo mwaka 2030. Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kutambua nafasi hiyo ya vijana wanatumia vijana wenyewe ili wawe mabalozi wa mashirika hayo mashinani ili kupigia chepuo yale yaliyomo kwenye SDGs.
Nchini Gambia, Magharibi mwa bara la Afrika, kalavati au daraja dogo lililojengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya mitaji, UNCDF kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU)ili kuunganisha maeneo mawili, Pakaliba na Baro Kunda, limesogeza huduma ya afya karibu na wakazi wa maeneo hayo.
Ikiwa ni siku 30 sasa tangu kuanza kwa mzozo huko Mashariki ya Kati, kati ya Israel na Wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas walioko katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Gaza, mashirika 18 ya Kimataifa ya misaada ya kibinadamu yametoa taarifa ya pamoja hii leo yakisema ‘i