António Guterres aunda Bodi ya Ushauri wa Kisayansi
Hatimaye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametimiza ahadi yake ya kuunda Bodi ya Umoja wa Mataifa ya Ushauri wa Kisayansi wakati huu ambapo teknolojia ya Akili Mnemba au ‘Artificial Intelligence’ imeshaanza kugonganisha vichwa vya watu kuhusu nafasi yake katika maendeleo duniani.&