Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kabrasha la Sauti

17 JANUARI 2023

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina na tunakupeleka nchini Belize, taifa la ukanda wa karibea kuona jinsi mabadiliko ya tabianchi yamesomba si tu nyumba bali pia makaburi. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kuhusu watoto katika kaya maskini, afya, na hatari zinazokumba wahamiaji.

Sauti
12'48"

16 JANUARI 2023

Ni Jumatatu tarehe 16 ya mwezi Januari mwaka 2023 na jaridani tunakuletea habari za machungu kutoka DRC pamoja na za kazi ya walinda amani nchini humo. Makala tunakuletea simulizi ya mkimbizi kuhusu safari kutoka Venezuela hadi Chile, na mashinani tunakwenda nchini Somalia, kulikoni?

Sauti
11'
TANZBATT 9 / Private Sosper Msafiri

TANZBATT 9 nchini DRC wahitimisha kampeni ya Amani na Afya kwa kukabidhi jengo

Kikosi cha 9 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupitia Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo - MONUSCO wamehitimisha kampeni yao ya Afya na Amani iliyoanza tarehe 3 mwezi huu wa January ambapo  wam

Sauti
3'55"