ILO yawasaidia wakimbizi kupata ajira nchini Jordan
Nchini Jordan changamoto ya wananchi, wakimbizi na hata wahamiaji kupata ajira imepata suluhisho baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kazi ulimwenguni, ILO, kuingia ubia na vyama vya ushirika vya kilimo wa kuunganisha wasaka ajira na wamiliki wa mashamba.