Umoja wa Mataifa na mashirika yake yawasaidia wananchi wa Haiti
Shirikia la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Haiti linakadiria watu milioni 1.2, wakiwemo watoto 540,000, wameathiriwa na tetemeko la ardhi na karibu watoto laki 5 hawana huduma ya malazi, maji safi na salama, pamoja na huduma za afya na lishe.