Michuano ya paralympic yaanza rasmi Tokyo Japan
Mashindano ya kimataifa ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu yameanza rasmi hii leo mjini Tokyo Japani yakihusisha washiriki wa michezo mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wakiwemo wakimbizi.
Mashindano ya kimataifa ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu yameanza rasmi hii leo mjini Tokyo Japani yakihusisha washiriki wa michezo mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wakiwemo wakimbizi.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa FAO limewaalika waandishi wa habari katika ziara ya siku nne mkoani kigoma nchini Tanzania ili kutembelea miradi yake hususan ya uvuvi Fish4ACP mkoani humo ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa mkoa huo na kwingineko.
Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo limetoa wito kwa kundi la Taliban linalishika hatamu hivi sasa nchini Afghanistan kuheshiimu haki za binadamu, sheria za kimataifa na kutozima matumaini ya raia wan chi hiyo.
(TAARIFA YA LEAH MUSHI)
Hii leo katika jarida utasikia kuanza kwa mashindano ya kimataifa ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu mjini Tokyo Japani yakihusisha washiriki wa michezo mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wakiwemo wakimbizi.
Mabadiliko ya tabianchi katika maeneo kadha ya ulimwengu ni dhahiri. Bwana Vincent Alpha Opion ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa wilaya ya Kikuube nchini Uganda anasema, hata katika eneo lao, tayari wameanza kukosa mvua ikilinganishwa na kipindi ambacho mazingira yalikuwa katika hali yake.
Katika mahojiano na Grace Kaneiya, Oscar Ikinya manusura wa shambulio la bomu la Kenya la mwaka 1998 ametupeleka nyuma miaka 23 iliyopita na kuelezea kilichotokea akisema miaka hiyo yote baaday ya shambulio hilo bado maisha yake sio kama alivyotarajia.
Tuliyokuandalia hii leo kutoka Umoja wa Mataifa:
Tuna habari muhimu za siku na katika mada yetu kwa kina tutaelekea nchini Kenya kukutana na manusura wa shambulio la bomu la Kenya la mwaka 1998.
katika kujifunza Kiswahili tunapata ufafanuzi wa maana na matumizi ya neno "MUHUNI" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.
Hii leo katika jarida utasikia mahojiano na manusura wa Covid-19, Bwana Ole Pertet, mmoja wa wakazi wa Marekani waliougua mwanzoni kabisa ugonjwa huo ulipoingia Marekani.
Katika baadhi ya jamii barani Afrika bado zipo tamaduni ambazo kwa kiasi kikubwa zinawakandamiza wasichana na pia wanawake ingawa ipo mikakati mingi ya kupambana na tamaduni hizo na matunda yanaanza kuonekana.