Wakimbizi wakumbuka machungu waliyopitia
Ikiwa leo ni miaka 70 tangu kusainiwa kwa mkataba wa kimataifa wa wakimbizi mwaka 1951, wanufaika wa nyaraka hiyo wanashukuru kwa kuwa bila nyaraka hiyo maisha yao yangalikuwa ya tabu .
Ikiwa leo ni miaka 70 tangu kusainiwa kwa mkataba wa kimataifa wa wakimbizi mwaka 1951, wanufaika wa nyaraka hiyo wanashukuru kwa kuwa bila nyaraka hiyo maisha yao yangalikuwa ya tabu .
Machafuko yanayoendelea huko Tambura jimbo la Equatoria magharibi nchini Sudan Kusini yamesababisha maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao na kwenda kuomba ulinzi katika kambi ya walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS.
Mkutano wa utangulizi kuhusu mifumo ya chakula ukiendelea mjini Roma, Italia, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo , IFAD limetoa wito wa mabadiliko kadhaa muhimu katika mifumo ya chakula, ikiwemo kujitolea kufadhili na pia dhamira ya kisiasa kuhakikisha watu wa vijijini wanawezeshwa
Kampuni ya uhandisi kutoka Thailand, HMEC, inayofanya kazi kwa pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS imepatia wakazi wa eneo la Yei mjini Juba mafunzo ya kilimo cha mazao ya chakula sambamba na mapishi kama njia mojawapo ya kujitegemea katika chakula.
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia Roma nchini Italia kunakofanyika mkutano tangulizi wa viongozi kuhusu mifumo ya chakula duniani, kisha anakwenda Sudan Kusini ambako huko walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Thailand wanatekeleza kauli ya wahenga kuwa mfundishe mtu kuvua samaki badal
Jaridani Julai 26, 2021 na Assumpta Massoi
Jaridani ni habari kwa ufupi na makala ya kina ikiangazia homa ya ini kuelekea siku ya homa ya ini ambayo huadhimishwa kila mwaka Julai 28. Na katika mashinani tutakuwa nchini Tanzania.
kujifunza lugha ya Kiswahili kupitia neno la wiki hii leo mchambuzi wetu ni kutoka nchini Uganda ambako Mwenyekiti wa Idara za Kiswahili za Vyuo Vikuu vya Afrika MAshariki Aida Mutenyo anafafanua maana ya neno BASI
Jaridani Ijumaa Julai 23, 2021-
Ikiwa leo ni Ijumaa tuna habari kwa ufupi na mada kwa kina ambayo ni simulizi ya muuguzi aliyepata COVID-19 na kisha kupona pia neno la wiki ambapo mchambuzi wetu anachambua neno "basi"
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na kutangazwa na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO, tayari umeweka wazi kuwa kumekuwa na upotevu mkubwa wa ajira duniani.
Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa na Umoja wa Mataifa na wadau kwa wafungwa 50 wanawake na wanaume kwenye mji mkuu Bangui, yameanza kuwapatia nuru wafungwa hao huku wakiwa na matumaini kuwa watakapokuwa huru, stadi hizo zitasaidia kujenga upya maisha yao.&