UN na serikali wataka msaada wa haraka, hali ya njaa Madagascar ni tete!
Msaada wa kibinadamu wa haraka unahitajika ili kuwanusuru wananchi waishio kusini mwa Madagascar ambao sasa wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame ulioikumba nchi hiyo.
Msaada wa kibinadamu wa haraka unahitajika ili kuwanusuru wananchi waishio kusini mwa Madagascar ambao sasa wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame ulioikumba nchi hiyo.
Hali ya njaa Madagascar ni tete! UN na serikali wataka msaada wa haraka.
Hospitali bila wauguzi ni sawa na gari bila injini, anasema Muuguzi Mildred Okemo.
Na mashirika ya UN yapambana na utapiamlo shuleni Guatemala.
Miongoni mwa malengo 17 endelevu ya umoja wa Mataifa ni lengo namba tano la usawa wa kijinsia linalolenga kuwainua na kuwasaidia wanawake na wasichana. Pwani mwa Kenya Salma Hemed ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa shirika la Haki Africa, amejitwika jukumu la kuhakikisha kuwa wanawake wanapa
Kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia kwa Mfuko wa Kichocheo cha Biashara Somalia, SBCF, kampuni ya Solargen kupitia umeme wa nguvu ya jua imefanikiwa kuleta unafuu wa kimaisha kwa wananchi wa Warsheikh, katika pwani ya Somalia. Anold Kayanda anaeleza zaidi.
Juhudi za kimataifa za kujikwamua kiuchumi na janga la corona au COVID-19 ziko katika tishio kubwa, huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka na utoaji wa chano katika nchi masikini ukidemadema na pengo la usawa likitumbukiza nyongo matarajio ya ukuaji wa uchumi kwa silimia 5.4 mwaka huu wa 20
Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa Michelle Bachelet ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na muendelezo wa ghasia katika maeneo yanayokaliwa ya wapalestina ikiwemo Yerusalemu mashariki na Israel katika siku za hivi karibuni. Taarifa ya Leah Mushi inaeleza zaidi.
Ghasia zaendelea Yerusalem Mashariki, UN yapaza sauti.
Juhudi za kujikwamua na COVID-19 zakumbana na kigingi, huku gonjwa wakiongezeka, imesema ripoti ya hali na matarahjio ya uchumi duniani, WESP.
Kupitia mada kwa kina ya Jarida la Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Leah Mushi anachambua faida za ndege wahamao, ambao huadhimishwa kila Jumamosi ya tarehe 8 Mei ikiwa ni njia mojawapo ya kutambua faida zao katika maisha ya binadamu na sayari dunia.
Katika mada kwa kina, vijana nchini Tanzania wamechukua hatamu ya maisha yao kwa kujiunga katika umoja ili kutekeleza azma ya Umoja wa Mataifa ya kuondokana na umaskini ifikapo mwaka 2030. Mwenyeji wetu katika mada kwa kina in Leah Mushi!Karibu!
Wanahabari wa kada mbalimbali nchini Tanzania, wamepatiwa mafunzo juu ya malengo namba 6, 7 na 13 ya maendeleo endelevu, kupitia shirika la Climate Network Tanzania, CAN lenye ufadhili wa mashirika ya umoja wa mataifa ikiwemo lile la mpango wa maendeleo, UNDP, ili kukabiliana na mabadiliko ya tab