28 Aprili 2021
Bei ya vifaa vya mtu kujipima mwenyewe VVU yashuka.
Watu milioni 29 wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi ukanda wa Sahel.
Na, Je unawezaje kuanza upya maisha ukiwa umepoteza kila kitu?
Bei ya vifaa vya mtu kujipima mwenyewe VVU yashuka.
Watu milioni 29 wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi ukanda wa Sahel.
Na, Je unawezaje kuanza upya maisha ukiwa umepoteza kila kitu?
Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ujulikanao kama MINUSCA, umeendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenye lengo la kupunguza athari za kimazingira kwa raia wa nchi hiyo hususan katika udongo, hewa na katika vyanzo vya maji. Taarifa ya Flora Nducha inaeleza.
Nchini Sudan Kusini, kwenye mji wa Aweil, vijana 40 wa kiume na wa kike wamesema wananufaika na mafunzo ya ufundi kwa miezi mitatu yanayotolewa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ambaye bado yuko ziarani kwenye ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika, amezishukuru Rwanda na Niger kwa kuwezesha utekelezaji wa mpango wa kuhamisha wasaka hifadhi wanaokumbwa na madhila nchini Libya.
Asante Rwanda kwa kukubali kunusuru wasaka hifadhi walio hatarini Libya, asema Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi.
UNMISS yatoa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa vijana wa Sudan Kusini.
Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP mwaka 2017 lilizindua kampeni ya bahari safi au CleanSeas kwa lengo la kushirikisha serikali, umma, mashirika ya kiraia na sekta binafsi katika kutokomeza utupaji taka kwenye maeneo ya bahari na maziwa.
Kuelekea siku ya malaria duniani Aprili 25, Grace Kaneiya akiwa Nairobi, Kenya amezungumza na Dkt. Dan James Otieno kutoka Shirika la afya ulimwenguni, WHO nchini Kenya katika programu ya malaria inayofanya kazi kwa pamoja na wizara ya afya nchini humo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya sayari mama dunia ambayo huadhimishwa kila tarehe 22 ya mwezi Aprili, amesema maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika wakati sayari iko katika hali mbaya wakati binadamu wanaendelea kunyanyasa ulimwengu wa asili.
Kutana na Alaa, mkimbizi kutoka Syria ambaye amemudu kuwahamasisha wanawake wenzake kutoka Syria na wenyeji wake Lebanon kutumia michezo na mazoezi ya mwili ili kujenga kujiamini na pia kujenga jamii hata wakati wa janga la COVID-19.
Katika kuelekea siku ya malaria duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Aprili, shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limepongeza idadi kubwa ya nchi zinazokaribia na kufikia, utokomezajhji kabisa wa malaria. Taarifa ya Jason Nyakundi inaeleza kwa kina.