Jamii na serikali wanaitikia wito wa huduma za uzazi wa mpango
Vikao vya ngazi ya juu vya Umoja wa Mataifa vikiendelea kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani, mashirika ya kiraia nayo yanashiriki katika vikao vya kando kuelezea kile ambacho yanafanya mashinani kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs huko mashinani.