Janga la njaa DRC ni zahma kubwa duniani:WFP
Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linaongeza kasi ya usaidizi wake kwenye eneo la kaskazini-mashariki kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususan jimboni Ituri kufuatia kuanza tena kwa mapigano ya kikabila yaliyosababisha makumi ya maelfu ya watu kukimbia makazi yao.