Kujitioa ICC sio sahihi: Ban
Tamko la nchi tatu za Afrika la kujitoa kwenye mkataba wa mahakama ya kimataifaya uhalifu ICC, linatuma ujumbe mbaya amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Tamko la nchi tatu za Afrika la kujitoa kwenye mkataba wa mahakama ya kimataifaya uhalifu ICC, linatuma ujumbe mbaya amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Ofisi yahakiza bunadmau ya Umoja wa Mataifa imelaani vitendo vinavyotekelezwa na kundi la kigaidi la ISIL kuwalazimisha mamia ya maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao katika wilaya karibu na Mosul na raia wengine kulazimishwa kuhamia ndani ya mji wenyewe tangu mapambano ya kivita yalianza tarehe 1
Wiki hii Umoja wa Mataifa umeadhimisha siku ya wafanya kazi wa Umoja huo. Wafanyi kazi katika sehemu mbali mbali kuliko ofisi za Umoja wa Mataifa wameadhimisha siku hii kwa njia mbali mbali.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi dhidi ya shule mashariki mwa mji wa Aleppo nchini Syria hii leo ambayo yamesababaisha vifo vya watu kadhaa.
Oktoba 24 ni siku ya Umoja wa Mataifa ambapo chombo hicho chenye nchi wanachama 193 huangazia shughuli zake zinazojikita katika misingi mikuu ya maendeleo, Amani na usalama na haki za binadamu.
Katika Neno la Wiki hii Oktoba 28 tunaangazia matumizi potofu ya wingi kwenye maneno yasiyopaswa kuwekewa wingi. Maneno hayo ni: uamuzi, kuboresha na saa. Mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, huko nchini Tanzania.
Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ni lazima itegemee ushirikiano baina ya nchi wanachama wake wala si mashindano, wamesema washiriki wa mjadala wa kisiasa uliofanyika wiki hii mjini Kigali nchini Rwanda kuhusu ukhirikiano wa kikanda.
Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema limesikitishwa mno na matukio ya jana usiku ambapo watoto wakimbizi wamelazimika kulala nje kwenye baridi baada ya kambi yao kuteketezwa moto huko Calais, Ufaransa.
Zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini Sierra Leone ikiwa ni watu milioni 3.5 wana uhaba wa chakula, na hawana uhakika wa chakula. Kati yao watu zaidi ya 600,000 hawana chakula bora.
Watoa misaada ya kibinadamu wanatupia jicho kwa karibu hali ya wakimbizi waliosahaulika na wa muda mrefu, lakini pia wakimbizi wapya katika ngazi ya kimataifa kwa lengo la kushughulikia changamoto zinazowakabili watu hao ambao kutwa wako safarini.