El-nino ikitarajiwa, WHO yasaidia kutokomeza kipindupindu Tanzania
Mvua za el-nino zikakribia katika ukanda wa Afrika Mashariki, serikali ya Tanzania imejizatiti kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu ambao unakabili mikoa 17 ya nchi hiyo.
Mvua za el-nino zikakribia katika ukanda wa Afrika Mashariki, serikali ya Tanzania imejizatiti kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu ambao unakabili mikoa 17 ya nchi hiyo.
Ugonjwa wa Ebola ulitikisa Sierra Leone kwa muda zaidi ya mwaka mmoja na kugarimu maisha ya zaidi ya watu 3,000.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni, UNESCO linaendesha warsha maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa washikadau mbali mbali wa sekta ya elimu nchini Kenya kwa lengo la kuboresha mifumo ya kidijitali kwa wanafunzi walio na ulemavu.
Vita vinavyoikumba Syria vimesababisha mamilioni ya watu kukimbia makwao na watoto wengi kuacha shule. Nchini Lebanon ambako kuna zaidi ya wakimbizi Milioni Moja wa Syria, mashirika ya kibinadamu yanahaha kutoa huduma za elimu kwa watoto wasyria 400,000 wenye umri wa kuandikishwa shuleni.
Katika mpango wa kuhakikisha kwamba watu wanaoishi mitaa duni wanawakilishwa na kuhusihswa katika maendeleo Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani kwa kushirikisha vijana limeungana na msanii Juliani ambaye ni kijana aliyekulia mtaa duni nchini Kenya lakini kubadilisha maisha yake kupitia
Wakati ambapo eneo la mashariki ya kati linakumbwa na dhoruba kali, ukanda wa Afrika Mashariki pia unakabiliwa na mvua nyingi, watalaam wakielezea kwamba hizo zimesababishwa na mabadiliko ya tabianchi ambayo husababisha halijoto ya maji ya bahari ya Pacifiki kupanda na mfumo wa mvua kubadil
Mkutano mkuu wa dunia kuhusu masafa ya mawasiliano ya radio umeingia siku ya Tano huko Geneva, Uswisi ukiwa na lengo la kuangalia upya sera kuhusu mgao na matumizi ya masafa.
Utamaduni ni jambo linalotambulisha jamii ya eneo fulani kwa wakati fulani. Kadri siku zinavyoenda, tamaduni ambazo zimekuwa zinatambulisha jamii fulani ziko hatarini kutoweka kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo utandawazi na ukosefu wa juhudi za kuhifadhi tamaduni hizo.
Kwa takribani wiki moja sasa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitia kamati zake limekuwa likipokea ripoti za wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki mbali mbali duniani. Miongoni mwao ni ripoti kutoka kwa Mutuma Ruteere,
Licha ya kuwa nchi inayoongoza kwa kilimo cha pamba duniani, ukosefu wa mitaji na sababu nyinginezo umesababisha taifa la India kutonufaika na mazao hayo kwani hayaleti tija kwa wakulima hususani wadogowadogo.