Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kabrasha la Sauti

Hali ya walimu Afrika Mashariki

Wakati ambapo jamii ya kimataifa imeadhimisha siku ya walimu duniani, hapo tarehe 5, Oktoba, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO limekariri wito wake wa kuhakikisha kwamba walimu wanaajiriwa wa kutosha na wanawezeshwa ili kuwapatia watoto wote duniani elimu bora.