Michezo kwa amani, maendeleo na furaha.
Michezo ikitumiwa vyema yaweza kuleta hamasa ya maendeleo na amani katika jamii licha ya faida nyinginezo ikiwamo mshikamano na afya kwa wale wanaojihusisha nayo.
Michezo ikitumiwa vyema yaweza kuleta hamasa ya maendeleo na amani katika jamii licha ya faida nyinginezo ikiwamo mshikamano na afya kwa wale wanaojihusisha nayo.
Ukatili wa kingono umekuwa tishio la maendeleo na ustawi wa wanawake na watoto hususan kwenye maeneo ya vita. Vikosi vya usalama na vile vilivyojihami hudaiwa kufanya vitendo hivyo ili kujenga hofu miongoni mwa jamii bila kujali kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema tangazo la serikali ya Kenya kutoa muda wa miezi mitatu kuifunga kambi ya wakimbizi Daadab na kisha kuwarudisha makwao wakimbizi wa Somalia zaidi ya 350,000 limewastua , na kuitolea mwito serikali ya Kenya kutafakari upya.
Ni lazima mataifa hususan yanayoendelea yawekeze katika sekta mbali mbali badala ya mafuta pekee ili kuweza kukabiliana na athari za kushuka kwa bei za mafuta hususan wakati huu ambao kunashuhudiwa kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo duniani.
Vuguvugu la nafasi ya asasi za kiraia katika maendeleo hususan namna bora ya matumizi ya rasilimali fedha linachukua kasi kimataifa amesema mmoja wa washiriki wa mkutano kuhusu uwezeshaji wa kifedha unaoendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Licha ya changamoto nyingi zikiwamo uitikio wa wananchi katika vita dhidi ya umaskini na baadhi ya wahudumu wa umma kujilimbikizia mali za kufadhili vita dhidi ya umaskini, Uganda inaendelea kupambana na umaskini.
Leo ikiwa ni miaka 21 baada ya kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Umoja wa Mataifa pamoja na Ujumbe wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja huo wameandaa kumbukizi maalum jijini New York, kwa ajili ya kukumbuka mateso dhidi ya watutsi na baadhi ya wahutu walioyoyapitia nchini Rwanda mwaka 1994.
Kurasimisha ajira zisizo rasmi mathalani vijana wanaotembeza bidhaa mikononi kwaweza kukuza sekta ya ajira, hiyo ni kauli ya waziri wa kazi na ajira wa Tanzania, Gudencia Kabaka katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii mjini New York.