Maadhimisho ya kimataifa ya kupinga ukeketaji
Tarehe Sita mwezi Februari kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake. Maadhimisho ya mwaka huu yanajikita katika kukomesha kitendo hicho kinachofanywa siyo tu na mangariba bali pia wahudumu wa afya wakiwamo wauguzi na madaktari.