Serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua ili kutokomeza mauaji dhidi ya albino
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Tanzania, Tom Bahame Nyanduga, amesema ni jukumu la serikali kuhakikisha kwamba watekelezaji wa mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wanapewa adhabu kali itakayozuia wengine kujiingiza kwenye vitendo hivyo vya kinyama.