DRC: Mlipuko wa volkano ya mlima Nyiragongo jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC ulisababisha Yvonne Mukendo apoteze njia ya kujipatia kipato. Lakini UN Women ilimwezesha kuanzisha upya biashara yake pamoja na ushoni na sasa anajengea uwezo wanawake wnengine kama yeye.
HONDURAS: "Nataka kuwa daktari", "Nataka kuwa mhandisi." ni baadhi ya ujumbe kutoka kwa watoto wa kike wanaopanda basi lililopatiwa jina Ruta de los Sueños au Njia ya Ndoto. Basi hilo mradi wa UNFPA husafiri maeneo ya kijijini kuelimisha kuhusu afya ya ngono na uzazi ili kuepusha mimba zisizohitajika.
UZBEKISTAN: Wanawake ni wanufaika wa mradi huu wa FAO ambapo kwenye mashamba yao kuna vihisishi vya kidijitali vilivyounganishwa kwenye intaneti kuwawezesha kudhibiti kiwango cha joto, unyevunyevu kwenye udongo na mwanga kwenye mabanda ya bustani na hivyo kongeza uzalishaji.
ETHIOPIA: Mkusanyiko huu wa kunywa kahawa huleta pamoja wanawake na wasichana walioathiriwa na vita na ambao wanahitaji huduma za matibabu, msaada wa sheria na kisaikolojia. Watoa huduma hizo hupatikana huku huduma ya kahawa ikiendelea.