Hapa, afisa uhusiano wa Syria Lt. Kanali Souad Kemal akisalimiana na mkuu wa wafanyakazi wa UNTSO Meja-Jenerali Carl C. von Horn mwaka wa 1959. Leo, walinada amani 150 wa kijeshi wa UNTSO wanaendelea kufuatilia usitishaji mapigano, kusimamia mikataba ya uwekaji silaha chini, na kuzuia matukio ya pekee ambayo yanaweza kusababisha vurugu na mzozo.
Walinda amani katika misheni zote 12 za sasa wanafanya kazi katika shughuli za kufikia jamii ili kusikiliza na kukidhi mahitaji ya kipekee ya idadi kubwa ya watu, kuanzia kuwatahadharisha watoto kuhusu hatari ya mabomu ya ardhini hadi elimu ya amani shuleni.
Takriban miaka 40 iliyopita, wanawake waliwakilisha asilimia 1 ya walinda amani, idadi ambayo ilipanda mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 4.8 ya vikosi vya kijeshi na asilimia 10.9 ya vitengo vya polisi vilivyoundwa. Leo, Umoja wa Mataifa unaendelea kufanya kazi na serikali kuimarisha uwakilishi wa wanawake. Jifunze zaidi kuhusu wanawake katika ulinzi wa amani hapa.
Katika Sahara Magharibi, mojawapo ya maeneo 17 kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa ya kukomesha ukoloni na miongoni mwa maeneo yaliyochafuliwa zaidi duniani kufuatia miaka 16 ya vita, ujumbe wa Umoja wa Mataifa, MINURSO, unasaidia kuondoa mabaki ya vifaa vya milipuko ambayvo havijalipuka vilivyosambaa katika eneo lenye mchanga lenye urefu wa kilomita 2,700. "Kwa kila bomu ninaloliondoa ardhini, nina imani kwamba nimeokoa maisha," anasema mtegua mabomu Fatimetu Bushraya Malainin, mwanamke wa Sahrawi aliyezaliwa katika kambi ya wakimbizi huko Tindouf, Algeria.
Askari wa kulinda amani ambao ni wataalam wa mifugo wanasaidia kulinda mifugo na maisha ya watu katika mazingira hatarishi, kupitia timu hii ya madaktari kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ambao wanasaidia wafugaji kwenye zahanati ya Abyei iliyoanzishwa kwa ajili ya wafugaji kuweka mifugo yao salama na yenye afya baada ya kupoteza maelfu ya Wanyama kwa magonjwa mapema 2023.
Baada ya mlipuko mbaya huko Beirut mwaka 2020 ambao uliua zaidi ya watu 200, UNIFIL ilisaidia mamlaka ya kitaifa kutathmini uharibifu na kusaidia juhudi za uokoaji, ikituma timu ya matibabu ya dharura. Jifunze jinsi walinda amani walivyosimama bega kwa bega na watu wa Lebanon hapa.
Pia walisaidia kusambaza vifaa muhimu, ikiwa ni pamoja na barakoa, bidhaa za usafi, na bidhaa za elimu kwa jamii za mashinani, kuanzia kuendesha kliniki za upimaji hadi huduma za ushafi shuleni. Jifunze jinsi walinda amani walivyochangia katika juhudi za kitaifa za kukabiliana na coronavirus hapa.
Nchini Syria, mlinda amani akisalimiana na wanafunzi katika Shule ya Faouar, mojawapo ya shule nne zilizorekebishwa na Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo (UNDOF) kama sehemu ya mradi wa athari za haraka unakabiliana na mahitaji ya dharura ya jamii za wenyeji. Miradi mingine kama hiyo imesaidia kuboresha barabara, madaraja, na hospitali ulimwenguni kote. Pata maelezo zaidi kuhusu miradi ya jumuiya hapa.
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakiwa katika doria kwenye masoko na vitongoji, kama afisa huyu wa Polisi wa Umoja wa Mataifa huko Timbuktu, akichunguza jamii zilizoathiriwa na ghasia katika eneo hilo. Jifunze kuhusu jinsi walinda amani wanavyojitahidi kulinda raia hapa