Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yatumia turufu kupinga ombi la Palestina kuwa mwanachama kamili wa UN

Balozi Robert A. Wood wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa akipiga kura ya turufu dhidi ya rasimu ya ombi la Palestina kutaka uanachama kamili UN
UN Photo
Balozi Robert A. Wood wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa akipiga kura ya turufu dhidi ya rasimu ya ombi la Palestina kutaka uanachama kamili UN

Marekani yatumia turufu kupinga ombi la Palestina kuwa mwanachama kamili wa UN

Masuala ya UM

Leo Baraza la Usalama limekataa ombi la Palestina la kutaka uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa, huku Marekani ikitumia kura yake ya turufu katika kura mahsusi iliyopigwa kuhusu ombi hilo.

Katika kura upigaji kura huo kulikuwa na kura12 za kuunga mkono moja ya kupinga na wanachama wawili wa Baraza walijizuia kutopiga kura. 

Kwa mantiki hiyo Baraza halikupitisha rasimu ya azimio ambalo lingependekeza kwa Baraza Kuu kupigiwa kura na wanachama wa Umoja wa Mataifa ili kuruhusu Palestina kujiunga kama mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa. 

Rasimu ya azimio hilo ni miongoni mwa rasimu fupi zaidi katika historia ya Baraza ikisema “Baraza la Usalama, baada ya kuchunguza maombi ya Taifa la Palestina kwa ajili ya kujiunga kama mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa (S/2011/592), linapendekeza kwa Baraza Kuu kwamba Taifa la Palestina kukubaliwa kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa."

Ili rasimu ya azimio kupitishwa, Baraza lazima liwe na angalau wajumbe tisa wanaounga mkono na kusiwe na wanachama wake wa kudumu ambao i China, Ufaransa, Urusi, Uingereza, Marekani wanaotumia kura yao ya turufu.

Uwasilishwaji wa ombila uanachama

Katikati ya vita inavyoendelea Gaza, Palestina ilikuwa imewasilisha ombi kwa Katibu Mkuu tarehe 2 Aprili, ikitaka ombi la mwaka 2011 la kuwa nchi mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa liangaliwe upya.

Mnamo mwaka wa 2011, Baraza la Usalama lilizingatia ombi hilo lakini halikuweza kupata umoja katika kutuma pendekezo kwa Baraza Kuu, ambalo kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa lazima lipige kura inayohusisha nchi zote 193 Wanachama wake.

Mapema mwezi huu, Baraza la Usalama lilituma ombi la hivi karibuni kwa Kamati yake ya kukubali nchi wanachama, iliyokutana tarehe 8 na 11 Aprili kujadili suala hilo.

Palestina imekuwa Mwangalizi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa tangu 2012, kabla ya hapo ilikuwa mwangalizi katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.