Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Fatou Haidara, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO na Mkurugenzi Msimamizi wa Idara ya Ubia wa Kimataifa UNIDO (kulia) akiwa na Abdulla bin Adel Fakhro,, Waziri wa Viwanda waBahrain kandoni mwa ufunguzi wa WEIF 2024, Manama, Bahrain
UNIDO-ITPO

WEIF2024 yaanza Bahrain ikilenga kuchochea ugunduzi na ujasiriamali

Jukwaa la tano la kimataifa la uwekezaji kwa ujasiriamali, WEIF2024 linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa limeanza leo huko Manama, Bahrain likiwa na wawakilishi wa serikali, mashirika ya kiraia, wawekezaji, wasomi na wabunifu na wakitoka pembe zote za dunia kwa lengo la kusaka mbinu za kuchochea ubunifu na ugunduzi ili hatimaye kusaidia kusongesha malengo ya maendeleo endelevu.