Nchini Zimbabwe asilimia 70 ya wakazi milioni 13 wa taifa hilo ni vijana wenye umri wa chini ya miaka 30 ambapo vijana wanne kati ya watano hawana ajira na sasa Umoja wa Mataifa umechukua hatua kuwanusuru.
Asilimia 38 ya watu wote wanaoishi vijijini nchini Zimbabwe sawa na takribani watu milioni 3.5 kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu wa mavuno Septemba 2019 hawana uhakika wa chakula kutokana na ukame wa mara kwa mara.