Katibu Mkuu Antonio Guterres, leo ametuma ujumbe maalumu wa mshikamano kwa waathitirika wa kimbunga IDAI , na serikali ya Msumbiji akiahidi kwamba kwa hali na mali Umoja wa Mataifa uko pamoja nao.
Atahari za kimbiunga IDAI Kusini mwa Afrika ikiwemo Zimbabwe na Malawi ni kubwa lakini nchini Musumbiji ni sawa na bomu linalosubiri kulipuka hususani katika masuala ya afya na usafi.
Watu zaidi ya 500 wamepoteza maisha Zimbabwe, Malawi na Msumbiji kutokana na mafuriko yaliyosabnabishwa na kimbuga IDAI na kuwaacha maelfu bila makazi wakihitaji msaada wa haraka wa kibinadamu. Leo mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa umetangaza dola milioni 20 kusaidia waathirika.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea kusikitishwa kwake na vifo, uharibifu wa mali na kufurushwa kwa watu kufuatia mvua kubwa na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Idai.