Zeid Ra’ad Al Hussein

Azimio kuhusu Ghouta Mashariki litekelezwe- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefungua kikao cha 37 cha Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo huko Geneva, Uswisi akitaka utekelezaji wa haraka wa sitisho la mapigano huko Syria baada ya Baraza la Usalama kupitisha kwa kauli moja azimio hilo.

Ukatili gani wasubiriwa ili hatua zichukuliwe huko Ghouta?

Syria hali inazidi kuwa mbaya zaidi , raia wanakabiliwa na mashambulizi. Tangu tarehe 4 mwezi huu wa Februari raia zaidi ya 300 wameuawa kwenye mapigano kati ya serikali na wapinzani.

Baada ya miaka 10 jela Teodora yu huru El Salvador

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa  leo imekaribisha habari za serikali ya El Salvador  kumuachilia huru mama aliyehukumiwa miaka 30 jela kwa kudaiwa kumuua mwanaye pale alipojifungua mtoto aliyekufa na ametolewa baada ya kuwa jela kwa miaka 10.

Sauti -
1'4"

Iran acheni kuwanyonga watoto mnakiuka sheria za kimataifa: Zeid

Kamisha Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein leo ameitaka serikali ya Iran kuheshimu, kuzinhatia sheria za kimataifa na kukomesha mara moja unyongaji wote wa watu waliohukumiwa kifo kwa makossa waliyoyatenda wakiwa watoto, barubaru au vijana wadogo.