Asanteni Umoja wa Mataifa mmetunusuru- Wanufaika wa miradi ya UN
Kuelekea maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 mwezi huu wa Oktoba, wanufaika wa miradi ya chombo hicho mashinani wamepaza sauti zao kutoa shukrani kwa jinsi maisha yao yamebadilika kutokana na miradi inayotekelezwa kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa.