Yemen

17-05-2019

Jaridani Mei 17 , 2019 na Assumpta Massoi

Katika habari kwa ufupi habari ikiwmeo-

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yamelaani mashambulizi ya anga yaliyofanyika jana Alhamisi kwenye mji mkuu wa Yemen, Sana'a.

Sauti -
9'55"

Idadi ya vifo na majeruhi Yemen inashtua-UN

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na lina hofu kubwa kufuatia ripoti za vifo vya raia na majeruhi wakati mashambulizi yalipoughubika mji wa Sana’a nchini Yemen jana Alhamisi

Hali Yemen iko njia panda llicha ya kuondolewa kwa waasi wa Houthi-Griffiths

Hali Yemen iko njia panda licha ya kuondolewa kwa waasi wa Houthi kutoka kwenye eneo la bandari la Hodeida ambalo ni muhimu kwa uwasililishaji wa msaada wa kibindamu amesema mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Martin Griffiths wakati wa kikao cha Baraza la Usalama hii leo juu ya Yemen.

UN yaunga mkono Mkataba wa Hodeida (UNMHA)

Vikosi vya Umoja wa Mataifa pamoja na vikosi vya ulinzi wa pwani nchini Yemeni  vimeanza doria rasmi ya maeneo ya bandari katika mji wa Hudayidah nchini Yemeni kufuatilia makubaliano kati ya majeshi ya Houthi yaliyo chini ya uongozi Ansar Allahna  na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa Hodeida (UNMHA).

WFP yafanikiwa kufikia kinu cha kusaga nafaka cha bahari ya Shamu Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP na timu ndogo ya mafundi  wa kampuni ya kusaga nafaka ya bahari ya Shamu ambayo ni muhimu katika usambazaji wa chakula kwa mamilioni ya watu nchini humo, wamefanikiwa kufikakwenye kinu hicho mwishoni mwa juma na sasa wanaendelea na shughuli ya kusafisha na kukarabati mitambo au mashine kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kusaga tena ngano na kusambaza kwa wahitaji.

Wahamiaji 8 toka Ethiopia wamefariki dunia wakiwa rumande katika hali mbaya Yemen:IOM

Wahamiaji takriban wanane kutoka nchini Ethiopia wameripotiwa kufariki dunia nchini Yemen ambako walikuwa wanashikiliwa mahabusu kwenye vituo maalum, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.

Yemen acheni kuadhibu watu kwa misingi ya imani zao- Wataalamu

Watalaam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka mamlaka zilizoko hivi sasa Yemen kutupilia mbali mara moja adhabu ya kifo aliyohukumiwa Hamid Kamali bin Haydara, kwasababu tu ya kuwa muumini wa dini ya Bahá’í.

"Ajabu na kweli," surua yashamiri hata kwenye nchi zinazoongoza kwa kutoa chanjo- WHO

Visa vya surua vimeendelea kuongezeka mwaka 2019 huku takwimu za mapema zikionyesha kwamba visa vilivyoripotiwa viliongezeka kwa asilimia 300 katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu wa 2019 ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka 2018.

Umoja wa Mataifa una wasiwasi na hali inavyoendelea Yemen

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo mjini New York, Marekani kujadili hali ya Yemen ambapo viongozi wakuu wa Umoja wa Mataifa wamelieleza baraza hilo kuhusu wasiwasi wao juu ya machafuko yanayozidi kuongezeka katika maeneo mengine ya Yemen na nje ya mji wa bandari wa Hudaidah ambako mkataba wa kusitisha mapigano unaendelea kutekelezwa.

Mlipuko waua watoto wengine 14 na kuwajeruhi 16 wakiwa shuleni mjini Sana’a.

Mkurugenzi wa shirika la Umoj awa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kanda ya Mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika, Geert Cappelaere kupitia taarifa iliyotolewa hii leo mjini Geneva, Sana’a na Amman Yemen, amesema mlipuko uliotokea mjini Sana’a jana umewaua watoto 14 na kuwajeruhi 16 wakiwa shuleni na wengi wao wakiwa chini ya umri wa miaka tisa.