Yemen

Hukumu ya kifo dhidi ya watu 30 sana’a inatutia hofu-OHCHR

Ofisi ya Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu imesema imeshtushwa na kutiwa hofu kubwa na hukumu ya kifo waliyokatiwa watu 30 na mahakama ya mwanzo maalum kwa makossa ya jinai mjini Sana’a nchini Yemen.

Kila tunakokimbilia na wanangu, ni kaburi-Mkimbizi Yemen

Mwezi huu tarehe 20, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP Limeanza kwa kiasi kuanza usitishaji wa msaada wa chakula nchini Yemen katika maeneo yaliyokaliwa na mamlaka zenye makao yao mjini Sana’a. Maamuzi hayo yamechukuliwa baada ya majadiliano kuchelewa kuhusu makubaliano ya kuanzisha udhibiti wa kuzuia chakula kuelekezwa kwingine badala ya kwenda kwa walengwa walioko hatarini.

WFP ‘yasitisha’ mgao wa chakula kwenye maeneo yanayodhibitiwa na wahouthi Sana’a

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limethibitisha hii leo kusitisha kwa kiwango kidogo mgao wa chakula kwenye maeneo yanayodhibitiwa na majeshi ya upinzani ya wahouthi nchini Yemen.

Zaidi ya wahamiaji 2000 wa Ethiopia warejea nyumbani kutoka Yemen:IOM

 

Wahamiaji zaidi ya 2100 raia wa Ethiopia wamerejea nyumbani kutoka Yemen kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.

Ghasia angalau zimepungua kidogo Yemen- Griffths

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili ya kisiasa na kibinadamu nchini Yemen ambapo mjumbe maalum wa umoja huo kwa Yemen Martin Griffiths amesema ghasia kwenye majimbo sita nchini humo zimepungua kufuatia pande husika kwenye mkataba wa Hudaydah kupunguza mapigano licha ya kwamba utekelezaji wa mkataba huo haujawa kikamilifu.

Mwanamke mmoja na watoto wachanga sita wanafariki dunia kila baada ya saa mbili nchini Yemen kutokana na matatizo ya ujauzito

Kila baada ya saa mbili mwanamke mmoja na watoto wachanga sita wanaozaliwa nchini Yemen wanakufa kutokana na matatizo wakati wa ujauzito au wakati wa kujifungua, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF hii leo mjini New York Marekani, Amman  nchini Jordan na na Sana’a Yemen.

Mambo yakizidi kuchacha Yemen wasomali Zaidi ya 4000 warejea nyumbani:UNHCR

Karibu Wasomali 4300 sasa wamerejea nyumbani kutoka Yemen tangu mchakato wa kuwasaidia wakimbizi kurejea nyumbani kwa hiyari ulipoanza kutekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR mwaka 2017.

Kuchelewa kuondoka kwa ndege za misaada ya kibinadamu kunawaweka hatarini wahamiaji nchini Yemen.

Taarifa iliyotolewa hii leo mjini Aden Yemen na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na wahamiaji IOM inasema zaidi ya wahamiaji waethiopia wanaoshikiliwa katika hali mbaya mjini Aden Yemen ilikuwa warejeshwe nyumbani kwa msaada wa shirika hilo katika operesheni iliyopangwa kuanza jumamosi ya wiki iliyomalizika yaani Mei 25, lakini zoezi hilo limecheleweshwa na marufuku ya shughuli za ndege katika eneo hilo.

WFP yafikiria kusitisha utoaji misaada sehemu zinazodhibitiwa na Houthi huko Yemen

Shirika la mpango wa chakula dunia WFP linataka mambo matatu ya dharura kufanyika nchini Yemen yakiwemo: uhuru wa kuhudumu, kuwafikia wale walio na njaa na kufanyika usajili wa kieletroniki.

Sauti -
1'33"