Katika ajenda ya maendeleo endelevu SDGs ya mwaka 2030, lengo namba 3 la afya bora kwa kila mtu, limekuwa changamoto kubwa sana hasa kwa nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la sahara.
Nchini Afghanistan, shambulio kwenye kitongoji cha Qalai Nazir karibu na mji mkuu Kabul, limesababisha watu wapatao 100 kuuawa na wengine wengi wamejeruhiwa.
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limefurahishwa na hatua ya malori yake 30 yaliyosheheni chakula na misaada mingine ya kibinadamu kufika mji wa Aweil nchini Sudani Kusini. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Tarehe 20 mwezi septemba mwaka huu 2017 mji wa Mexico nchini Mexico ulikumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.1 katika kipimo vya richa na kusababisha vifo vya Zaidi ya watu 200 na kuharibu mamia ya majengo.