Tarehe 24 mwezi Oktoba kila mwaka ni siku ya Umoja wa Mataifa, siku ya kusherehekea kuasisiwa kwa katiba ya kuanzisha Umoja wa Mataifa mwaka 1945 baada ya vita kuu ya pili ya dunia.
Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya usaidizi nchini Afghanistan, UNAMA, imelaani vikali shambulio la leo kwenye msikiti mmoja huko Maimana katika jimbo la Faryab nchini humo lililosababisha vifo vya 4o na wengine 56 wamejeruhiwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ametaka vurugu zilizoanza upya kwenye jimbo la Rakhine nchini Myanmar zikomeshwe mara moja na amezisihi mamlaka nchini humo kuchukua hatua kumaliza vurugu hizo.