Marais watatu kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika ya Magharibi ECOWAS wamewasili mjini Abijan Ivory Coast kumshawishi Rais Laurent Gbagbo kukubali kushindwa na kuondoka madarakani.
Kamishna wa amani na usalama katika muungano wa afrika AU Ramtane Lamamra pamoja na balozi wa china nchini Ethiopia Gu Xiaojie wametia sahihi makubaliono ambapo China itatoa misaada kwa kikosi cha kulinda amani nchini Somalia cha AMISON.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani kwenye jimbo la Darfur (UNAMID) kimeeleza hisia zake kunapoendelea kushuhudiwa mapigano kati ya vikosi vya jeshi la Sudan na makundi ya waasi kwenye maeneo yanayokumbwa na ghasia.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani ghasia zilizoshuhudiwa katika sehemu kadha nchini Nigeria katika siku za hivi maajuzi na kusababisha vifo vya watu 30 huku wengine zaidi ya 70 wakijeruhiwa.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amelaani shambulizi la kigaidi lililotekelezwa nje ya kituo cha kusambaza misaada cha shirika la mpango wa chakula duniani WFP mashariki kwa Pakistan ambalo lilisababisha watu 45 na kuwajeruhi wengine wengi.
Wafuasi wanaomuunga mkono mshindi wa uchaguzi wa rais nchini Cote d\'Ivoire ambaye anatambuliwa kimataifa Allasane Ouattara wameitisha mgomo wa kitaifa nchini humo, kumlazimisha rais anayeng\'ang\'ania madarakani Laurent Gbagbo kuachia madaraka.
Rais mpiganaji wa Ivory Coast ambaye amegoma kuondoka madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi ametakiwa kutimiza ahadi yake na kutoendeleza ghasi.
Ni miaka isiyozidi mitano iliyosalia kabla ya 2015 muda ambao ni kikomo cha utekelezaji wa malengo yote manane ya maendeleo ya milenia yaliyoafikiwa na viongozi wa dunia mwaka 2000. Burundi ikiwa ni mmoja wa wao