Women, children, population

UM kuandaa kongamano la ujenzi mpya wa Pakistan baada ya mafuriko

Shirika la umoja wa mataifa linaloratibu misaada ya usamaria mwema UNOCHA likishirikiana na benki ijulikanayo Pakistan JS Bank Limited linaandaa kongamano maalumu kwa ajili ya kuijenga upya Pakistan

Fedha bado ni tatizo siku 100 baaya ya mafuriko Pakistan

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa siku 100 baada ya mafuriko kuikumba Pakistan kwa sasa mamilioni ya watu wanahitaji usaidizi wa dharura.

Ugaidi bado ni tishio kubwa Kusini Mashariki mwa Asia:UM

Ugaidi bado unatajwa kuwa tisho kubwa kusini mashariki mwa Asia hata baada ya mitandao ya kigaidi kupata pigo kufuatia ushirikiano uliopo wa kuzuia mashambulizi ya kigaidi.

UNHCR yatoa wito kuwalinda wakimbizi wa Kisomali kenya

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea kusikitishwa kwake kuhusu hatima ya zaidi ya wakimbizi 8000 kutoka Somali walioamrishwa kuondoka eneo la Mandera lililo kaskazini mashariki mwa Kenya mnamo juma hili.

Msaada wa dharura wahitajika kukabili kimbunga Tomas:OCHA

Umoja wa Mataifa unatoa wito wa misaada zaidi ya dharura pamoja na vifaa kwa taifa la Haiti wakati kimbunga Tomas kinapokaribia kuweasili nchini humo.

Polio yaripotiwa kuzuka DR Congo:WHO

Mkurupuko wa ugonjwa wa Polio umeripotiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku visa ya maambukizi 120 na vifo 58 vikiripotiwa.

UM watangaza duru nyingine ya mazungumzo Sahara Magharibi

Awamu nyingine ya mazungumzo kati ya pande zinazo zozana Sahara Magharibi itafanyika mjini New York juma lijalo kwa mwaliko wa Umoja awa Mataifa.

UM waeleza matatizo yanayokumba miji duniani

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lililo na jukumu la kuboresha miji ameelezea changamoto zinazokumba miji sehemu mbali mbali duniani akisema kuwa miji mingi ina idadi kubwa ya wakaazi ambao haina uwezo wa kuwahudumia.

Ban awataka viongozi wa Guinea kujiepusha na ghasia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa Guiene kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa wiki.

Licha ya kupungua utapia mlo, njaa bado ni tatizo:FAO

Umoja wa Mataifa leo unasherehekea siku ya kimataifa ya chakula ambayo kwa kawaida huadhimishwa tarehe 16 Oktoba duniani kote.