UNICEF inakadiria kwamba zaidi ya watu milioni 2 wangali wanaathiriwa moja kwa moja au kwa njia nyingine na matokeo ya mtetemeko wa ardhi huko Haiti. Na watu wengine milioni 1.3 wamekoseshwa makazi yao hadi hivi sasa.
Wakurugenzi wakuu wa Idara ya kuwahudumia watoto UNICEF na Mpango wa Chakula Duniani WFP wametoa wito kwa jumuia ya mataifa hii leo kuongeza msaada wao kwa waathiriwa wa mafuriko yanayoendelea huko Pakistan.
Idara ya Maendeleo kwajili ya Wanawake ya Umoja wa Mataifa UNIFEM, inaanda warsha mwezi mzima wa Septemba, katika wilaya saba za uchaguzi nchini Tanzania ili kuimarisha mikakati ya uchaguzi ya wagombea wanawake, kabla ya uchaguzi mkuu wa October.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linakutana hii leo kuzindua rasmi Mpango wa Kimataifa wa Kuchukuliwa Hatua kupambana na biashara haramu ya binadamu. Akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu Ban Ki-moon anasema biashara haramu ya watu ni miongoni mwa ukiukaji mbaya kabisa wa haki za binadamu.
Shirika la afya Ulimwenguni WHO linakadiria kwamba zaidi nusu ya milioni ya kina mama wajawazito ambao wamekumbwa na mafuriko nchini Pakistan watajifungua katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kuongeza juhudi zao ili kuendelea na ahadi ya kuokoa maisha ya wanawake na watoto.
Makala yetu ya wiki hii inamulika juu ya Mkutano wa kimataifa wa vijana unaofanyika huko Leon Mexico. Wajumbe kutoka zaidi ya serikali mia moja pamoja na mashirika yasio ya kiserikali, Umoja wa Mataifa na vijana wanahudhuria mkutano huo na kujadili juu ya masuala mbali mbali yaliyomuhimu kwa vijana
Rais Mwasi kibaki wa Kenya aliidhinisha katiba mpya wakati wa sherehe za kihistoria zilizofanyika Ijumaa asubuhi kwenye uwanja wa Uhuru mjini Nairobi na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa kutoka mataifa jirani, wapatanishi wa mzozo wa Kenya pamoja na maelfu ya wananchi.