Women, children, population

Walimwengu waandamana kuunga mkono juhudi za WFP kupiga vita njaa duniani

Ijumapili ya tarehe 07 Juni (2009) makumi elfu ya watu, katika sehemu mbalimbali za dunia, walikusanyika kwenye miji kadha ya kimataifa, na kuandamana kuunga mkono juhudi za Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) katika kupiga vita tatizo la njaa ulimwenguni, hususan miongoni mwa watoto wadogo.

FAO yatoa mwito wa kubuniwa mfumo imara dhidi ya njaa

Jacques Diouf, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) ametoa mwito maalumu, uitakayo jamii ya kimataifa kuimarisha mfumo wa utawala bora wa kukabiliana na matatizo ya njaa, kwa kuhakikisha akiba ya chakula katika ulimwengu itadhaminiwa kwa taratibu zitakoridhisha na kutimiza mahitaji ya chakula ya muda mrefu kwa umma wa kimataifa.

Wawakilishi wa tamaduni za kijadi Afrika Mashariki wazingatia kikao cha mwaka juu ya haki za wenyeji wa asili

Wiki hii tutakamilisha makala ya pili ya yale mahojiano yetu na wawakilishi wawili wa jamii za makabila ya wenyeji wa asili kutoka Afrika Mashariki, ambao karibuni walihudhuria kikao cha nane cha ile Tume ya Kudumu ya UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili Duniani kilichofanyika Makao Makuu.

Hali ya usalama wa kigeugeu Kivu Kaskazini inaitia wasiwasi OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti hali ya usalama wa raia, ulioregarega Kivu Kaskazini, inaitia wasiwasi mkubwa wahudumia misaada ya kiutu waliopo katika JKK.

Uhamisho wa raia Usomali unaendelea kukithiri wakati mapigano yakishtadi

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti idadi ya raia waliolazimika kuyahama makazi katika mji wa Mogadishu, tangu mapigano kuanza mnamo tarehe 08 Machi (2009), imekiuka watu 96,000 kwa sasa.

UN-HABITAT/UNIFEM yatashirikiana kupiga vita udhalilishaji na utumiaji mabavu dhidi ya wanawake

Mashirika mawili ya UM, yaani lile shirika juu ya makazi, UN-HABITAT, na lile shirika linalohusika na mfuko wa maendeleo kwa wanawake, UNIFEM, yameshirikiana rasmi kujumuika bia kukabiliana na tatizo la udhalilishaji na matumizi ya mabavu dhidi ya wanawake na watoto wa kike, katika miji ya mataifa yanayoendelea.

IFAD inayahimiza mataifa Afrika kukipa kilimo umuhimu kupambana na matatizo ya fedha

Kanayo F. Nwanze, Raisi wa Shirika la UM linalohusika na ukomeshaji wa ufukara na umaskini wa vijijini, yaani Shirika la Kimataifa juu ya Maendeleo na Kilimo (IFAD) ameshauri kwamba serikali za Afrika, zenye kutunza na kuhudumia kimaendeleo sekta ya kilimo, ndizo zitofanikiwa kudhibiti, kwa wastani, athari mbaya zinazoletwa na migogoro ya fedha duniani.

Zimbabwe itahitajia dola milioni 719 kuhudumia kidharura umma

UM imeripoti Zimbabwe inahitajia wahisani wa kimataifa kuchangisha msaada wa dharura, kwa mwaka huu, unaokadiriwa dola milioni 719 kukidhi mahitaji ya kiutu kwa umma na kufufua uchumi nchini, baada ya shughuli hizo kuporomoka nchini karibu miaka kumi.

Mjumbe Malumu kwa Sudan ameingia wasiwasi juu ya usalama wa kusini

Kadhalika, baada ya ziara ya siku mbili Sudan Kusini, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan, Ashraf Qazi, ambaye vile vile ni Mkuu wa Shirika la Ulinzi Amani la UM kwa Sudan Kusini (UNMIS) alisema ameingiwa wasiwasi juu ya kuharibika kwa hali ya utulivu kwenye eneo hilo mnamo miezi ya karibuni, kwa sababu ya mapigano ya kikabila yaliofumka kwenye majimbo ya Nile ya Juu na Jonglei.