Women, children, population

Hapa na pale

Rachel Mayanja, Mshauri Maalumu wa KM kuhusu Masuala ya Kijinsia na Maendeleo ya Wanawake amependekeza kwa jamii ya kimataifa kubuniwe kanuni za kukabiliana na vitendo haramu vya kutumia mabavu na kujamii kwa nguvu wanawake kwenye mazingira ya vita, na alitaka vitendo hivi vitafsiriwe kama uvunjaji sheria wa kiwango cha juu wenye kuvuka mipaka ya maadili ya kiutu.~

Migiro atoa mwito wa kukithirisha uekezaji dhidi ya vifo vya uzazi

Naibu KM Asha-Rose Migiro aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano wa London kuhusu haki za wanawake na afya bora ya kuwa wakati umeshawadia kwa walimwengu kutimiza ahadi ya kuekeza mitaji ya maendeleo katika huduma za kustawisha afya na hali njema kwa wanawake kote duniani, ikijumuisha pia udhibiti wa vifo vya uzazi. Alionya Naibu KM kwamba bila ya kuyafanya haya mataifa yote, kote duniani, hayatofanikiwa abadan kujiepusha na athari za umasikini na hali duni.

Juhudi za Kimataifa za kupiga marufuku mila ya kukeketwa wasichana kote duniani

Watalamu kutoka sehemu mbali mbali za dunia pamoja na wajumbe wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, makundi ya kidini, mashirika yasiyo ya kiserekali, maafisa wa idara za usalama na wa serekali, walikutana mjini Addis Abeba mapama mwezi wa Agosti kutathmini na kujadili njia za kukomesha kabisa mila ya kukeketa wasichana.

Utumizi wa musiki katika kuhamasisha watu juu ya masuala ya kijamii

Mwaka 1954 Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF lilianza kuomba msaada wa watu mashuhuri hasa wasani, waimbaji na wachezaji michezo tofauti kutumia uwezo na umashuhuri wao kuhamasisha watu juu ya haki za watoto na masuala mengine yanayo husiana na watoto. Mtu wa kwanza alikua Danny Kaye aliyekua mtumbuizaji na msani mashuhiri sana aliyefariki 1987 akiwa balozi wa nia njema wa UNICEF.

Katibu Mkuu ameitisha mkutano wa aina ya pekee kuimarisha maendeleo Afrika

Ripoti ya mwezi Juni (2007) ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) ilibainisha mataifa ya Afrika yaliopo kusini ya Sahara bado yamepwelewa sana kwenye juhudi za maendeleo, kwa ujumla, na hakuna dalili haya yatafanikiwa kuyakamilisha, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ya kupunguza kwa nusu, kabla ya 2015, umasikini, njaa, maradhi na kutojua kusoma na kuandika.

Mkutano wa Kamati ya Kuondowa kabisa Ubaguzi dhidi ya Wanawake

Kamati ya Kuondowa kabisa Ubaguzi dhidi ya Wanawake, iliadhimisha miaka 25 ya kufuatilia utekelezaji wa mataifa wa makubaliano hayo ya kihistoria mwishoni mwa mwezi wa juli kwa kikao cha siku tano hapa Umoja wa Mataifa.

Mkutano wa Kamati ya Kuondowa Ubaguzi dhidi ya Wanawake

Kamishna mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi Louise Arbour hivi karibuni alipongeza kazi za Kamati ya Kuondowa kabisa Ubaguzi dhidi ya Wanawake, inapoadhimisha miaka 25 ya kufuatilia utekelezaji wa mataifa wa makubaliano hayo ya kihistoria.

Ukuaji wa Idadi ya Watu huko Tanzania

Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa, Christopher Mwaijonga mwakilishi mkazi msaidizi huko Tanzania, amesema kwamba, wakati wa mkutano wa Cairo juu ya Idadi ya Watu, 1994, wajumbe walisisitiza juu ya kuwekea mkazo juu ya kuwapatia uwezo wanawake kuamua wakati wanapotaka kupata mimba na kuimarisha afya ya uzazi.

Kazi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu UNFPA huko nchini Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA hufuata sera ya kushirikiana na nchi husika kupanga mahitaji muhimu ya nchi hiyo. Huko Tanzania, shirika hilo linazingatia maeneo matatu muhimu, Afya ya uzazi, Suala la Jinsia hasa kwa kuongeza uwezo wa kina mama kufanya maamuzi, na mwisho ni juu ya idadi ya watu na maendeleo.

Mkuu wa huduma za dharura wa UM yuamulika atahri za ukame huko Kusini mwa Afrika.

Mratibu wa huduma za dharura wa UM, Bw John Holmes alimulika wiki hii atahri za ukame sugu unaokumba nchi kadhaa za Kusini mwa Afrika, akisisitiza kwamba hali ni mbaya zaidi huko Swaziland. Alisema wanatarajia matatizo makubwa ya ukosefu wa akiba ya chakula katika eneo hilo.