Women, children, population

UM umewataka vijana kuwa msitari wa mbele kuleta maelewano

Mkutano wa pili wa Kimataifa uliowahusisha vijana wenye ushawishi kwenye jamii zao umemalizika katika Mji Mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur, kwa kutolewa mwito kwa vijana hao kuongeza sauti zao ili kukaribisha hali ya maelewano.

Vikwazo vya Israel ni adha kubwa Gaza:WFP na OCHA

Ripoti ya pamoja ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP na shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA inasema vikwazo vya ardhini na baharini vya Israel dhidi ya ukanda wa Gaza vina athari kubwa za kibinadamu.

UM kutathmini athari na msaada wa mafuriko Pakistan

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa alasiri ya leo linatathimini athari zilizosababishwa na mafuriko nchini Pakistan na msaada unaohitajika kwa mamilioni ya waathirika.

Leo ni siku ya kimataifa ya wahisani, wanajitolea kwa ajili ya wengine

Leo ni siku ya kimataifa ya wahisani ambao hujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wengine.

UM kutumia michuano ya Olimpiki kuwaasa vijana kuhusu ukimwi

Umoja wa Mataifa umetangaza mpango maalumu unakusudia kuongeza msukumo wa uelewa kwa vijana dhidi ya maambukizi ya Virusi vya HIV ambao wanabeba asilimia 40 ya maambukizi hayo, pamoja na kupiga vita vitendo vya unyanyapaa.

Mfuko wa UM watoa dola milioni 27 kusaidia Pakistan

Mamilioni ya watu walioathirika na mafuriko nchini Pakistan watapokea msaada wa haraka kufuatia dola milioni 27 zilizotolewa na mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF.

Sekta ya afya Afghanistan inahitaji kuwezeshwa:WHO

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahisani mwakilishi maalumu wa shirika la Afya duniani WHO nchini Afghanistan Peter Graaff amesema sekta ya afya nchini Afghanistan imeomba kuimarisha uwezo wa kuwafikia maelfu ya raia wan chi hiyo wanaohitaji msaada wa huduma ya afya.

IOM kuakabiliana na ukimwi kwa wahamiaji Afrika

Shirika linalohusika na uhamiaji la kimataifa IOM kanda ya kusini mwa africa kwa ushirikiano na shirika la kimataifa kuhusu mandeleo nchi Sweden (sida) pamoja na wizara ya mambo ya kigeni nchini Norway yametangaza upanuzi wa ushirikinao katika harakati za kukabiliana na virusi vinavyosababisha maradhi ya ukimwi hadi africa masharuiki.

Mizozo ni kikwazo kwa kufikia malengo ya milenia UM

Miaka mitano kabla ya mwaka 2015 ambao ni mwaka wa wa kutimizwa malengo ya ya milenia ya umoja wa mataifa, suala hilo linaokekana kutatizwa na changamoto zikiwemo za huduma mbaya za kiafya, vifo na kuwepo kwa pengo katika kutimiza malengo hayo.

UNDP inajiandaa kuisaidia Haiti katika uchaguzi ujao

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP linajiandaa kuisaidia Haiti katika masuala ya uchaguzi baada ya kukumbwa na tetemeko kubwa mapema mwaka huu.