Mwigizaji mashuhuri ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Academy ya nchini Marekani, Geena Davis amevitaka vyombo vya habari kuonesha umuhimu wa mwanamke katika jamii ili kufikia lengo la nane la maendeleo ya milenia, ifikapo mwaka 2015.
Kiongozi wa tume maalum ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan, ameikaribisha bodi huru iliyoteuliwa kusimamia maandalizi ya kura ya maani ambayo itashuhudia kujitenga ama la, kwa Sudan Kusini.
Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres ambaye yuko ziarani nchini Kyrgystan ametoa wito wa kuendelea kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa ndani nchini humo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameipongeza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo leo imeadhimisha miaka 50 ya uhuru waliounyakua kutoka kwa Wabelgiji.
Wafanyakazi wa misaada kwenye jimbo la Darfur Magharibi mwa Sudan wanasema mapigano yanayoendelea baiana ya makundi mbalimbali yenye silaha yameongezeka tangu mwezi Mai.