Wawakilishi kadha wa kimataifa walikusanyika kwenye Makao Makuu ya UM kuanzia tarehe 30 Juni kuhudhuria kikao cha mwaka cha Kamati ya Kuondosha Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW), kwa madhumuni ya kufanya mapitio juu ya namna Mataifa Wanachama yalioridhia Mkataba wa CEDAW yanavyowatekelezea wanawake haki zao. Miongoni mwa Mataifa manane yaliowakilisha ripoti za mapitio mbele ya Kamati mwaka huu, kwenye kikao cha 41, ilijumuisha pia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.