Women, children, population

Mkuu wa huduma za dharura wa UM yuamulika atahri za ukame huko Kusini mwa Afrika.

Mratibu wa huduma za dharura wa UM, Bw John Holmes alimulika wiki hii atahri za ukame sugu unaokumba nchi kadhaa za Kusini mwa Afrika, akisisitiza kwamba hali ni mbaya zaidi huko Swaziland. Alisema wanatarajia matatizo makubwa ya ukosefu wa akiba ya chakula katika eneo hilo.

Siku ya idadi ya watu

Dunia nzima iliadhimisha siku ya kimataifa ya idadi ya watu chini ya mada “wanaume kama washirika wa afya ya uzazi”. Sherehe mbali mbali zilifanyika kote duniani na abdushakur ana ripoti kamili.

Siku ya Idadi ya Watu Duniani

Katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon na mkurugenzi mkuu wa Idara ya Idadi ya Watu UNFPA, Bi Thoraya Ahmed Obaid waliadhimisha siku ya Idadi ya Watu, kwa kutoa mwito wa kushirikishwa zaidi wanaume katika afya ya uzazi ili kupunguza idadi ya wanawake wanaofariki kila siku wanapojifungua na kuhakikisha malezi ya usalama. Abdushkaur Aboud ana maelezo zaidi juu ya siku hii. ~~

UNICEF yapongeza Misri kupiga marufuku kukeketwa wasichana

Shirika la watoto la umoja wa mataifa UNICEF limepongeza hatua kadhaa zilizochukuliwa na Misri wiki iliyopita kuondowa mila ya kukeketwa wasichana, baada ya kufariki kwa msichana mwenye umri wa miaka 12 kutokana na kukeketwa.