Women, children, population

Makampuni ya madawa yaombwa na KM kushirikiana kimataifa kudhibiti vyema homa ya A(H1N1)

KM Ban Ki-moon kwenye risala yake mbele ya kikao cha 62 cha Baraza Kuu la Afya Duniani, kilichofunguliwa rasmi mapema wiki hii mjini Geneva, aliyahimiza makampuni yenye kutengeneza madawa kushirikiana na serikali wanachama katika kutafuta suluhu ya dharura, ili kuulinda ulimwengu na maambukizi hatari ya mripuko wa karibuni wa maradhi ya homa ya mafua ya A(H1N1).

Ripoti ya 26 ya WHO juu ya Homa ya A(H1N1)

Wataalamu wa kimataifa wametoa taarifa inayohadharisha kwamba ikiwa walimwengu hawatofanikiwa kudhibiti bora maambukizi ya homa ya mafua ya virusi vya A(H1N1), yanayotendeka miongoni mwa wanadamu, inaashiriwa katika miezi sita hadi tisa ijayo, kuna hatari ya maradhi haya kupevuka na kuwakilisha "janga jipya hatari la afya ya jamii kimataifa".

Mjumbe wa UM kwa Usomali ashtumu mashambulio ya Mogadishu dhidi ya serikali

Mjumbe Maalumu wa UM kwa Usomali, Ahmedou Ould- Abdallah ameshtumu vikali kuendelea kwa mashambulio dhidi ya wawakilishi wa Serikali halali ya Usomali na uhariibifu wa mali za serikali unaofanyika kwenye mji wa Mogadishu.

Makisio ya UM kuhusu hali katika jimbo la NWFP, Pakistan

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti hali kwenye eneo la mapigano la Jimbo la Mpakani Pakistan katika Kaskazini-Magharibi (NWFP) inashuhudia muongezeko mkubwa wa mateso kwa raia walionaswa katikati ya mapigano.

Mashirika ya WFP/WHO yahudumia kihali raia waathirika wa mapigano Sri Lanka

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa ilani inayohadharisha kwamba pindi halitafadhiliwa msaada wa dharura wa dola milioni 40, kuhudumia chakula umma ulioathirika na mapigano katika Sri Lanka, litashindwa kununua chakula, kuanzia mwisho wa Julai ili kunusuru maisha ya wahamiaji.

Makundi yanayopigana Sri Lanka yatakiwa kuhishimu usalama wa raia

Verinoque Taveau, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) aliwaambia waandishi habari Geneva kwamba makundi yanayopambana katika Sri Lanka, yaani vikosi vya Serikali na waasi wa kundi la LTTE [Tamil Tiger], yamenasihiwa na UNICEF kufanya kila wawezalo kuwahakikishia raia ushoroba wa kupita, bila ya kushambuliwa kwenye mazingira ya uhasama.

Uwekaji mipaka Abyei wazingatiwa na mahakama ya PCA

Mnamo Alkhamisi,07 Mei (2009) Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi, au Mahakama ya PCA, iliopo kwenye mji wa Hague, Uholanzi, ilimaliza kusikiliza hoja za watetezi wanaowakilisha makundi mawili yanayohusika na uwekaji mipaka rasmi ya ule mji wa Abyei, uliotawanyika kwenye eneo la kaskazini na kusini katika Sudan.

UNICEF imehadharisha, siasa za kigeugeu na vurugu vyahatarisha njaa kwa watoto wa Pembe ya Afrika

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limehadharisha ya kuwa mchanganyiko wa matatizo sugu ya chakula na hali iliopamba ya kigeugeu cha kisiasa kieneo, yanahatarisha ustawi na maisha ya mamilioni ya jamii ya watoto wanaoishi kwenye eneo la Pembe ya Afrika.

Riporti ya WHO kuhusu maambukizi ya homa ya H1N1

Takwimu mpya za maambukizo ya homa ya mafua ya A(H1N1) ulimwenguni, zilizothibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo Ijumaa ya tarehe 08 Mei (2009) ni kama ifuatavyo: Jumla ya watu 2500 waliripotiwa rasmi kuambukizwa na homa ya mafua ya H1N1 katika mataifa 25, ikijumlisha Brazil, kwa mara ya kwanza tangu tatizo hili la afya kuzuka.

UNICEF yaanzisha Zimbabwe kampeni ya ulinzi dhidi ya utoroshaji watoto

Shirika la Kimataifa juu ya Uhamiaji (IOM) pamoja na UNICEF, yameanzisha kampeni ya miezi mitatu Zimbabwe, iliokusudiwa kuimarisha hifadhi bora kwa watoto na uhamaji ulio salama.